Kongamano la Siku Maalum Dhidi ya Rushwa Katika Maonyesho ya SABASABA

0
451

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika amesema hatua zimeanza kuchukuliwa ili kudhibiti mianya ya Rushwa katika Biashara ila kuchochea Dira ya maendeleo ya Taifa.

Akizungumza katika Kongamano la siku maalum dhidi ya rushwa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara Julai 3,2019 yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Mkuchika amesema tafiti zinaonyesha Tanzania impiga hatua katika kudhibiti rushwa na kutaja maeneo ambayo serikali imeanza kufanya kazi ili kuendelea kupambana na Rushwa.