Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 43 yamezinduliwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara kutatua vikwazo vya biashara na uwekezeji nchini ili kuweka mazingira rafiki ya kuelekea uchumi wa viwanda na kusisitiza sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo kuhakikisha kunakuwa na malighafi zakutosha kwa ajili ya viwanda
Amesema maonesho ya Sabasaba ni maonesho makubwa katika ukanda wa kati.