Ashikiliwa kwa Kukutwa na Sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania

0
432

Jeshi la polisi Mkoani Morogoro linamshikilia Abubakari Makarabure mkazi wa Kihonda manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kukutwa na sare za jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro ,kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo Willbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea majira ya saa saba mchana katika kata ya Chamwino ambapo mtuhumiwa huyo alikutwa amevalia sare hizo ikiwemo shati moja,suruali moja ,kofia na viatu pea moja.

Akizungumzia tukio hili,kamanda Mutafungwa amesema mtuhumiwa huyo alikutwa katika kata ya Chamwino akiwa amevaa sare hizo za jeshi na kujitambulisha kwa vijana mbalimbali kuwa yeye ni afisa wa jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ nakuwaomba fedha ili aweze kuwasaidia kujiunga na jeshi hilo