Zaidi ya Vijiji Saba Wilaya ya Chunya na Songwe Vyanufaika na Pori la Akiba la Lukwati/Piti

0
412

Vijiji saba vinavyozunguka hifadhi ya Akiba ya Lukwati /Piti  katika wilaya ya Songwe  na Chunya  vimenufaika na utalii wa uwindaji  baada ya kujengewa  zahanati na shule  kutokana  na asilimia  25 % ya mapato yanayotokana na uwindaji huo.

Wananchi hao kutoka  Vijiji vya Ngwala ,Itiziro ,Kapalala na Gua  katika Mikoa ya Mbeya na Songwe  wamesema kujengwa kwa miradi hiyo hususani zahanati na shule kumesaidia kuondoa kero za muda mrefu  kwa wananchi  kutembelea umbali mrefu kufuata  huduma hizo muhimu katika maeneo mengine.

Meneja wa pori ,Jembe  Grispo  kutoka mamlaka ya usimamizi wanyama pori Tawa  anaelezea umuhimu wa pori hilo kwa wananchi.

Taarifa ya misaada hiyo imeungwa mkono na wakurugenzi wa halmashauri ya Chunya  Sophia Kumbuli na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Songwe Fauzia Hamidu.