Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wawekezaji zaidi kuwekeza jijini Dodoma

0
434

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kongamano la uwekezaji Dodoma na kusema kuwa mji huo ni mahali sahihi na pazuri kwa uwekezaji.

Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji jijini Dodoma lenye lengo la kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji katika jiji hilo.

Akifungua kongamano hilo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wawekezaji kuwekeza katika mkoa wa Dodoma kwani kuna mazingira rafiki ya uwekezaji.

Awali mawaziri kutoka wizara mbalimbali wameeleza adhma ya serikali katika kusimamia suala la uwekezaji nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge ametaja sifa zinazoufanya mkoa wa Dodoma kuvutia wawekezaji.

Kongamano la Uwekezaji Dodoma linaenda na kauli mbiu isemayo “DODOMA FURSA MPYA YA KIUCHUMI TANZANIA, WEKEZA DODOMA TUKUFANIKISHE.