Hatimaye Pamba yapata mnunuaji

0
458

Kampuni ya S&C Ginning Company Limited ya Bunda, Mkoani Mara, imetangaza kuanza kununua pamba za wakulima mkoani Katavi, baada ya kuwepo kwa kukata tamaa kwa wakulima wa zao la Pamba katika maeneo mengi nchini.

Mkaguzi wa Bodi ya Pamba mkoani Katavi Alfred Chagula, amewaambia wadau wa Kilimo katika Mkutano wa wadau hao unaoendelea Mjini Mpanda, Kampuni hiyo itanunua tani 15 milioni ya Pamba na Mkoa wa Katavi umezalisha zaidi ya Kilo 14 Milioni ya Pamba msimu huu.

Hofuu na wasiwasi iliyokuwa imewakumba wakulima wengi wa zao la Pamba mkoani Katavi imeanza kupotea, baada ya kuwepo kwa taarifa za kuanza tena kwa ununuzi wa pamba.

Katika Kikao cha wadau wa Kilimo mkoa wa Katavi, Bodi ya Pamba ikatoa taarifa ya kuanza tena kwa ununuzi wa zao la Pamba kwa bei elekezi ya shilingi 1,200 kwa kilo.

Mwakilishi wa Kampuni ya S&C Ginning Company Limite Mohonda Manyonyoryo amewahakikishia wakulima kuwa Pamba yao yote iliyozalishwa mkoani Katavi  itanunuliwa.

Kuanza kwa mara nyingine soko la Pamba mkoani Katavi Mkuu wa mkoa huu Juma Homera kawapongeza kampuni ya S&C kwa hatua hiyo na akaielekeza ijenge kiwanda mkoani humu.

Baadhi ya wakulima wameeleza kufurahia kwao lakini wakatoa changamoto ya soko la Pamba kila mwaka.