Sakata la utoroshaji Madini

0
254

Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia watu Wawili wanaodaiwa kukamatwa na madini aina Nane tofauti yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 958 yaliyokamatwa katika Barabara ya Arusha-Nairobi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Jonathan Shana akizungumza na waandishi wa Habari amesema madini hayo yenye uzito wa Kilo 31.59 na Karati 27.24 ambayo yalikuwa yamefungwa kwenye mifuko 74.

Pia amesema Askari walibaini madini hayo ambayo yalikuwa yanasafirishwa na gari lenye namba za usajili T716 ACC basi la kampuni ya Parfect.

Kamanda Shana amewataka wote wanaohusika na mzigo huo kujisalimisha kwajeshi la polisi.