Iran yatangaza Kuvunja Mkataba wa Amani

0
263

Mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea kati ya nchi ya Marekani na Iran, hauna dalili ya kupatiwa ufumbuzi, baada ya nchi ya Iran kutangaza kuwa sasa inaona kuwa inalazimika kuvunja mkataba wa amani wa nchi hiyo wa mwaka 2015.

Iran imetoa tangazo hilo baada ya serikali ya Marekani iliyotangaza kutoutambua mkataba huo wa kimataifa na kuahidi kuiwekea Iran vikwazo, kuanza kutekeleza vikwazo hivyo dhid ya baadhi ya viongozi wa serikali ya Iran.

Jana Iran ilitangaza kuwa haiko tayari kwa mazungumzo na Marekani, kwani nchi hiyo haimaanishi kile inachokizungumza. Nchi hizo katika siku za hivi karibuni zimekuwa zikitupiana maneno makali kutokana na mkataba wa mpango wa nyuklia wa Iran.