Watu 39 Wakamata kwa Tuhuma za Kuhusika na Mauaji ya Maafisa wa Jeshi

0
211

Polisi nchini Ethiopia wamewakamata watu 39 kutoka katika chama cha Impala cha nchini humo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya maafisa watano wa jeshi katika jaribio lililoshindwa la serikali katika jimbo la Amhara.

Watu wengine kadhaa waliuawa katika jaribio hilo lililoshindwa la mapinduzi ya serikali katika jimbo hilo. Mazishi ya watu hao waliokufa katika jaribio hilo la mapinduzi yamefanyika katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Ethiopia.

Wananchi wa nchi hiyo wanaendelea na siku tatu za maombolezo kutokana na vifo vya watu hao, akiwemo mkuu wa majeshi ya Ethiopia, na aliyekuwa gavana wa jimbo la Amhara.