Majeshi ya serikali ya mpito nchini Libya yamesema yameutwaa mji wa Garian ulioko nchini humo, ambao awali ulitekwa na majeshi yanayomuunga mkono mbabe wa kivita nchini humo Khalifa Hafter.
Hata hivyo wapiganaji wa Hafter wamekanusha taarifa hizo na kusema kuwa bado wanaudhibiti mji huo. Kumekuwa na mapigano makali kati ya askari wanaomuunga mkono Khalifa dhidi ya majeshi ya serikali ya mpito ya nchi ya Libya.
Wapiganaji hao walianza mashambulio mapya dhidi ya majeshi ya serikali ya mpito ya Libya, baada ya kutangaza kuwa yanakwenda mjini Tripol kutwaa madaraka na kuwaangamiza wapiganaji wa kikundi cha IS waliokuwa wamebaki nchini humo.