Madini yakamatwa Arusha yakitoroshwa

0
219

Polisi mkoani Arusha wamekamata kilo kadhaa za madini zilizokuwa zikitoshwa kwenda nchi jirani.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathani Shana amesema madini hayo yalikuwa yakisarishwa kwa basi kuelekea nchini Kenya.

Kamanda Shana amesema kazi ya kupima kilo sahihi za madini hayo inaendelea chini ya usimamizi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, polisi na wataalamu wa madini.