Picha ya Baba na Binti yenye majonzi tele

0
245

Picha ya baba na binti yake waliokufa maji katika mto unotenganisha nchi ya Marekani na Mexico, wakiwa njiani kwenda Marekani kutafuta maisha mazuri, imeangaza na kuleta picha ya matatizo wanayokabiliana nayo wakimbizi wakijaribu kuingia nchini humo.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 27 akiwa na binti yake mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja walikufa maji baada ya kusombwa na mkondo ndani ya mto huo alipokuwa akijaribu kuongelea.

Mke wa mtu huyo, mara baada ya kuona maji yamemzidi aliamua kugeuka na kurudi katika fukwe za Mexico. Hata hivyo rais Donald Trump wa Marekani ameendelea na mpango wake wa kutaka kupinga kura ya turufu kupinga wahamiaji kuingia nchini humo na kuwekewa bajeti ya fedha za matumizi.