Mbunge kutoka Kenya Jimbo la Starehe, Charles Njagua maarufu kwa jina la ‘Jaguar’ amekamatwa na Polisi kutokana na maneno yake ya chuki aliyoongea kuhusu raia wa Kigeni nchini Kenya
Jaguar alionekana kwenye video iliyosambaa katika mtandao ya kijamii akiwaambia wananchi wa Kenya kuwatoa kwa nguvu wafanyabiashara wa kigeni katika jimbo lake endapo hawataondoka na kufunga biashara zao.
Baada ya kushindwa kuripoti katika Kituo cha Polisi cha Bunge,Jaguar amekamatwa leo hii na kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Nairobi Area
Serikali ya Kenya imeweka msimamo wake wazi kuwa haijakubaliana na harakati za Mbunge huyo zakutaka kuwaondoa wafanyabiashara wa kigeni nchini humo