Taifa Stars kujipanga dhidi ya Harambee Stars

0
475

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wamesema watapambana ili waweze kushinda mchezo ujao  dhidi ya Kenya ili kuweza kujiweka kwenye mazingira mazuri kwenye michuano ya AFCON.

Mshambuliaji Simon Msuva na mlinzi wa kushoto Gadiel Michael wamesema mchezo huo dhidi ya Kenya ni muhimu mno kwao na ili kuweza kuibua matumaini lazima washinde.

Mchezo dhidi ya Kenya utachezwa kesho kutwa Alhamis ambapo timu zote mbili zilipoteza michezo yake ya kwanza ya hatua ya makundi hivyo zinataka kushinda  mchezo huo ili kuibua matumaini ya kubaki kwenye michuano hiyo.