Rais Donald Trump aweka vikwazo dhidi viongozi wa Iran

0
389

Serikali ya Iran imesema hatua ya Rais Donald Trump kuweka vikwazo dhidi ya baadhi ya viongozi wakuu wa nchi hiyo inafunga kabisa jitihada za kidiplomasia katika kutatua mgogoro baina ya mataifa hayo.

Mapema hapo jana Rais Donald Trump alitangaza kuwa Marekani imeweka vikwazo kwa viongozi hao akiwemo kiongozi mkuu wa kiimani nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei pamoja na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Javad Zarif, ambapo vikwazo hivyo vitadumu kwa muda wa mwaka mmoja.

Marekani imeweka vikwazo hivyo kwa viongozi hao ikiwa ni hatua ya nchi hiyo kuishinikiza Iran kuachana na  mpango wa kuendeleza urutubishaji wa madini ya Urani na utengenezaji wa silaha za nyuklia.