Rais Dkt. John Magufuli amesema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha nishati ya gesi inasambazwa kwa wingi ndani ya nchi
Akizungumza na wananchi jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua ghala na mtambo ya LPG ya TAIFA GAS, Rais Dkt. Magufuli amesema wakati umefika kwa watanzania kuzalisha gesi kwa wingi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Taifa Gas Mhandisi Hamisi Ramadhani amesema mahitaji ya gesi kwa sasa ni makubwa ndani na nje ya nchi na kuahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha mradi huo unakuwa na mafanikio kwa Taifa.
Kampuni ya gesi ya Taifa imeagizwa kusambaza kwa wingi gesi ili kuhakikisha inapatikana nchi nzima na kuwataka watanzania kutumia gesi hiyo ambayo matumizi yake ni nafuu.