Fernando Torres, amewahi kucheza timu mbali mabali kama Atletico Madrid, Liverpool ,AC Millan, Chelsea na Sagan Tosu vilevile Fernando alishinda Kombe la Dunia kwajili ya Hispania akiwa mchezaji muhimu wa kikosi cha Ushindi wa Kombe la Dunia 2010.
Fernando alitangaza Ijumaa katika ukurasa wake wa twitter
“Nina kitu muhimu sana chakutangaza. Baada ya miaka 18 ya kusisimua, wakati umefika wa kumaliza safari ya kazi yangu ya mpira wa miguu, “Torres alisema kwenye Twitter yake
Fernando Torres anaumri wa miaka 35 na sasa anacheza mpira Sagan Tosu iliyopo Japan.
Alicheza mara 334 Atletico, akifunga mabao 111. Torres pia na alifunga mabao 45 katika mechi 172 kwa Chelsea.
