Waandishi wa habari Myanmar wahukumiwa kifungo jela

0
2273

Mahakama nchini Myanmar imewahukumu waandishi wa habari wawili wa shirika la habari la Reuters kifungo cha miaka Saba jela kila mmoja kwa kosa la kufanya uchunguzi wa siri nchini humo kuhusu mgogoro wa Rohingya.

Waandishi hao ambao ni Wa Lone na Kyaw Soe Oo walishitakiwa kwa kosa la kuwa na nyaraka za serikali ambazo walidai kupatiwa na askari polisi, jambo ambalo wamedai lilikuwa limepangwa.

Kesi hiyo imeonekana kwa wengi kuwa ni ukandamizaji wa uhuru wa habari nchini Myanmar.

Waandishi hao walikuwa wanatafuta ushahidi juu ya mauaji wa wanaume Kumi yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo katika kijiji cha Inn Din In mwezi September mwaka 2017.