Maelfu Hong Kong waandamana na kukusanyika nje ya makao makuu ya jeshi la polisi

0
261

Maelfu ya wananchi wa Hong Kong wameandamana na kukusanyika nje ya makao makuu ya jeshi la polisi, kushindikiza kufutwa kabisa kwa muswada tata wa kutaka kusafirishwa kwa watu wa Hong Kong wanaokabiliwa na makosa mbalimbali kwenda kushitakiwa katika mahakama za China.

Taarifa kutoka Hong Kong zinaarifu kuwa hatua hiyo ya waandamanaji hao wameamua kukusanyika nje ya makao makuu ya jeshi hilo kwa kuwa lilitumika kuwatawanya walipoanza maandamano ya awali ya kupinga muswada huo mara ulipowasilishwa na mtendaji mkuu wa Hong Kong Carrie Lam ambaye pia alitangaza kusitiswa kwa muswada huo.

Hata hivyo Polisi wa Hong Kong wametaka waandamanaji hao kuondoka katika maeneo ya jeshi hilo,imesema uwepo wao katika maeneo hayo kuweza kusababisha matumizi ya nguvu ya ziada ya kuwatanya na kusabaisha ghasia.