Ndege isiyokuwa na rubani Iran yaendelea kuzua kizaza

0
291

Jeshi la Iran limeitungua ndege isiyokuwa na rubani ya jeshi la Anga la Marekani baada ya ndege hiyo kuripotiwa kuruka katika anga ya Iran.

Akizungumzia hatua hiyo baada ya kutunguliwa kwa ndege hiyo inayodaiwa ilikuwa ikitumika kukusanya taarifa za kijasusi dhidi ya Iran, Rais Donald Trump wa Marekani amesema Iran imefanya kosa kubwa sana kuitungua ndege hiyo na kuzidisha hali ya wasiwasi ya kuzuka kwa vita kati ya Marekani na Iran.

Taarifa zaidi kutoka Marekani zinaarifu kuwa, tayari Rais Donald Trump ameonyesha dhamira ya kuanzisha mashambulizi dhidi ya Iran,baadhi ya viongozi wa chama cha upinzani cha Democrat nchini humo akiwemo Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi wamesema Marekani haina sababu ya kuanzisha mashambulizi dhid ya Iran na kumtaka Trump kuzingatia ushauri kabla ya kuanzisha mapigano.

Kwa upande wake Balozi wa Iran katika umoja wa mataifa Majid Ravanchi amesema Iran haiko tayari kuanzisha vita dhidi ya Marekani na kusema kuwa jeshi la Iran liliitungua ndege hiyo ya marekani isiyokuwa na rubani baada ya kuingia katika anga la Iran, na kukaidi tahadhari zilizotolewa na jeshi hilo kabla ya kutunguliwa kwa ndege hiyo.