Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amelitaka shirikisho la soka hapa nchini (TFF) kuhakikisha fedha inayopatikana kwenye kuichangia Timu ya Taifa ya soka (Taifa Stars) itumike ipasavyoa kwenye kuwapa motisha wachezaji.
Makamu wa Rais ameyasema haya katika harambee maalum iliyofanyika leo ambapo wadau mbalimbali walipata nafasi ya kuichangia Timu hiyo inayojiandaa na Fainali za AFCON huko nchini Misri zinazotarajia kuanza kufanyika hapo kesho.
Siku moja kabla ya kuanza kwa michuano ya AFCON wadau hawa wa soka wamekutana kwa lengo la kuichangia timu ya Taifa (Taifa Stars).
Kiasi cha shilingi Milioni 370 zimepatikana katika Harambee hii kwa njia ya ahadi pamoja na fedha taslimu na hapa megni wa Rasmi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anasisitiza juu ya kamati kuhakikisha fedha hizo zinatumika kama zilivyokusudiwa.
Kwa upande wake waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr Harison Mwakyembe ametolea ufafanuzi wa nini timu hiyo inachangiwa badala ya serikali kubeba mzigo wote.
Baadhi ya wadau walioshiriki katika harambee wanasema hii ni ishara nzuri kwa timu kufanya vizuri katika Fainali za AFCON.
Harambee hii imefanyika siku mbili kabla ya Taifa Stars kushuka dimbani kupambana na Senegal kwenye mchezo wake wa kwanza wa michuano ya AFCON baada ya miaka 39 kupita.
