Mashambulio ya Anga Katika Uwanja wa Ndege wa Jizan uliopo Saudi Arabia

0
248

Wapiganaji wa kikundi cha Houthi cha nchini Yemen kwa mara nyingine wamefanya mashambulio ya anga katika uwanja wa ndege wa Jizan ulioko nchini Saudi Arabia, ikiwa ni hatua ya pande hizo mbili kuendelea kushambuliana.

Marekani imesema ina taarifa ya kutokea kwa mashambulio hayo na inafutatilia kwa karibu mgogoro unaoendelea kati ya wapiganaji hao na majeshi ya serikali ya Saudi Arabia.

Wapiganaji wa kikundi cha Houthi wanasema wanalipiza kisasi kwa vile mara kadhaa majeshi ya Saudi Arabia yakishirikiana na majesh ya nchi washirika yamekuwa yakifanya mashambulio nchini Yemen na kuwaua raia wasiokuwa na hatia.