Shirika la Utangazaji Tanzania TBC limepokea Tuzo ya kuwa chombo cha habari namba moja katika kurusha na kutangaza vivutio vya utalii nchini na kupewa Tuzo kutoka kwa TANAPA,Tuzo hiyo imepokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dr. Ayub Rioba katika hafla iliyofanyika Jijini Arusha