Kukamalika Uunganishaji wa Bomba la Maji Kutoka Ziwa Victoria

0
228

Katika kuhakikisha kuwa wananchi waishio maeneo ya Mjini wanapata asilimia 95 ya huduma ya maji safi na salama na asilimia 85 kwa wanaoishi vijijini ifikapo mwaka 2020 serikali inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya Maji ukiwamo mradi mkubwa wa kutoka ziwa Victoria kwenda katika wilaya za Igunga, Nzega, Uyui na Manispaa ya Tabora mkoani Tabora.

Naibu katibu mkuu wa wizara ya Maji Mhandisi Emmanuel Kalobelo amekagua utekelezaji wa mradi huo na kuwataka wananchi kuhakikisha kuwa huduma ya maji safi na salama wanayopatiwa na serikali iwe chachu ya kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii

Hatimaye unganishaji wa bomba katika eneo la kijiji cha Solwa mkoani Shinyanga liltakalopeleka maji katika wilaya za Igunga, Nzega, Manispa ya Tabora na Uyui  mkoani Tabora kutoka kwenye bomba kuu la maji linalotoa maji Ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kahama na Shinyanga imekamailika Utekelezaji wa mradi huo wa kimkakati umepokelewa kwa furaha na baadhi ya wananchi walioshuhudia kazi ya kutoboa bomba kuu nakuunganisha linaloelekea mkoani Tabora

Naibu katibu mkuu wa wizara ya Maji Mhandisi Emmanuel Kalobelo ambaye ameshuhudi hatua za mwisho za uunganishaji wa bomba hilo amewataka wananchi kuyatumia maji wanayopata kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Pia Naibu katibu mkuu wizara Mhandisi Kalobelo ameshauri kujengwa mifumo ukaosaidia uendeshaji na kutambua hitilafu zinazoweza kutokea katika mradi huo.