Riporti ya kuhusiana na mauaji ya mwandishi wa habari na mwanaharakati

0
234

Taarifa kuhusiana na uchunguzi wa kifo cha mwandishi wa habari na mkosaji mkubwa wa serikali ya Saudi Arabia, Ahmad Khashogg, unaonyesha kuwa serikali ya nchi hiyo ilihusika na kupanga kifo chake.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya uchunguzi kuhusiana na mazungumzo yaliyorekediwa ndani ya Ubalozi wa Saudi Arabia, mjini Istanbul nchini Uturuki, kuhusiana na kuharibu mwili, muda mfupi kabla ya Ahmad Khashogg kuingia na kisha kuuawa

Mwandishi habari Ahmad Khashogg na mwanaharakati maarufu aliyekuwa akiikosoa serikali ya Saudi Arabia, aliyeuwawa nchini Uturuki.

Mwandishi huyo wa habari Jamal Ahmad Khashogg aliuwawa baada ya kuingia kwenye ubalozi mdogo wa nchi yake ulioko mjini Istabul nchini Uturuki. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mauaji ya Khashogg ndani ya ubalozi huo yalikuwa yamepangwa.

Awali nchi ya Saudi Arabia ilikanusha kuhusika na kifo cha Khashogg, lakini kadri nchi ya Uturuki ilivyokuwa ikitilia mashaka tukio hilo na kutoa vielelezo vya awali, hatimaye nchi hiyo ilikiri kuwa mwanaharakati huyo aliuawa ndani ya ubalozi.

Hata hivyo hadi leo mwili wa Khashogg haujulikani ulipo, kwani haujapatikana, ingawa kuna tetesi ya kumwagiwa tindikali na kuyeyushwa.