Umoja wa Mataifa walaani matumizi ya watoto katika mashambulio ya mabomu

0
313

Umoja wa mataifa umelaani matumizi ya watoto wadogo katika mashambulio ya mabomu ya kujitoa muhanga kama mchango

Hatua hiyo ya Umoja wa mataifa inafuatia matukio ya milipiko ya kujitoa muhanga iliyotokea  katika kijiji cha Konduga kaskazini mwa Nigeria  na kusabasisha vifo vya watu takribani thelathini.

Tayari jeshi la polisi nchini humo linamshikilia mtu mmoja anayedaiwa kuhusika na milipuko hiyo huku kundi la Boko haram likidaiwa kuhusika kupanga mashambulio hayo.