Mazishi ya Rais wa zamani Cairo

0
254

Mazishi ya mwili wa Rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi yamefanyika mapema asubuhi ya leo mjini Cairo.

Taarifa za mazishi ya Morsi aliyefariki jana baada ya kuanguka mahakamani, zimetolewa na mtoto wake wa kiume Ahmed Morsi ambaye amesema mwili wa baba yake umezikwa katika makaburi walipozikwa baadhi ya viongozi wakuu wa chama Muslim Brotherhood.

Mazishi hayo ya Rais huyo wa zamani wa Misri aliyeingia madarakani kwa kuchaguliwa na wananchi wa Mirsi mwaka 2012 na kuondolewa madarakani July 2013 na jeshi la nchi hiyo, yamethibitishwa na mwanasheria wake Abdel Masoud.