Marekani imesema mazingira ya biashara nchini Tanzania ni ya kutabirika na hivyo imeipongeza serikali kwa kutatua changamoto mbalibali ambazo zilikuwa zinaathiri shughuli za uwekezaji.
Akizungumza katika mkutano wa wafanyabiashara wa Marekani jijini Dar es Salaam, balozi wa nchi hiyo Imni Patterson amesema Tanzania inamazingira ya biashara yanayotabirika ambayo yanafanya shughuli za uwekezaji kufanyika kwa tija.
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Uwekezaji,Angellah Kairuki na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania imechukua hatua mbalimbali zikiwemo za kisera katika kuboresha mazingira ya biashara Tanzania