Aliyekuwa Rais wa Misri Mohamed Moris amefariki dunia ghafla hii leo baada ya kuanguka akiwa Mahakamani kusilikiza mashtaka mbalimbali yanayomkabili.
Moris ambaye alichaguliwa kuongoza Misri mwaka 2012 kupitia chama cha Udugu wa kiislamu, aliondolewa madarakani na jeshi la nchi hiyo mwezi July mwaka 2013 kufuatia maandamano makubwa ya wananchi wa Misri kumtaka ajiuzulu.
Taarifa za kifo cha Rais huyo wa zamani wa Misri Mohammed Morsi zinaarifu kuwa, kabla ya kufikwa na umauti, kiongozi huyo alikanguka na kuzimia baada ya kuahirishwa kwa shughuli za mahakama na baadaye alifariki Dunia.
