Watu Saba Mbaroni Kisa Dawa Ya Kulevya

0
257

Jeshi la polisi kitengo cha kuzuia na kudhibiti dawa za kulevya linawashikilia watu 7 kwa tuhuma za kusafirisha, kusambaza na kuuza  dawa za kulevya.

Akizungunza na waandishi wa habari jijini DSM kamishna msaidizi wa polisi – ACP

 Salim Kabaleke amesema mtuhumiwa wa kwanza Rajab Mchigama(27) ambae ni dereva bodaboda alikamatwa mkoani Mtwara akisafirisha kilo 8 za Heroine na kufanikisha kukamatwa kwa wenzake 6

Kamishna Kibaleke amesema watuhumiwa wote wamekiri kuhusika na makosa hayo na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika ambapo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo ili kutokomeza biashara ya dawa za kulevya 

Kamishna Kibaleke amesema katika kipindi cha miezi sita iliyopita, jeshi hilo lomekamata zaidi ya kg 30 za dawa za kulevya aina ya Heroin vile vile Kamishna Kibleke amesisitiza kuwa uteketezwaji wa vielelezo vyote hufanya kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi pamoja na usalama wa wananchi.