Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewaonya mameneja wa tanesco wanaoagiza vifaa vya umeme nje ya nchi kinyume na makubaliano ya ununuzi wa vifaa ambavyo vinavyopatikana nchini kuacha mara moja tabia hiyo kwani inachelewesha miradi kukamilika kwa wakati
Waziri Kalemani ametoa kauli jijini Dodoma katika mkutano na mameneja wa TANESCO wa Wilaya,Mkoa ,Kanda, pamoja na wakala wa nishati vijijini REA mkutano unaolenga kufanya maboresho katika usambazaji nishati kwa wananchi.
Kuhusu utendaji na usimamizi mbovu katika usambazaji na uunganishaji wa umeme kwa wananchi,nalo waziri amelizungumzia.
Waziri Kalemani pia amebaini kuwepo kwa mahusiano yasiyo mazuri kati ya mameneja na wateja ama hata kwa mamlaka za maeneo wanayotekeleza miradi ya umeme.