Mapigano ya kikabila DRC ya sababisha vifo

0
264

Zaidi ya watu Mia Moja na Sitini wameuawa katika mapigano ya kikabila, mapigano yaliyozuka kwenye eneo la Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo – DRC.

Maafisa wa Jeshi la DRC wamesema kuwa mapigano hayo yaliyotokea katika vijiji vilivyopo kwenye jimbo la Ituri, yamechochewa na Wanamgambo wanaoongozwa na mtu anayejulikana kama Ngudjolo.

Habari zaidi kutoka katika Jamhuri hiyo ya Kidemokrasi ya Kongo zinasema kuwa wengi wa watu waliouawa wanatoka kwenye kabila la Hema.

Kwa muda mrefu, watu wa kabila la Hema ambao ni wafugaji wa Ng’ombe na wale wa kabila la Lendu ambao ni ya Wakulima, wamekua katika mapigano ya kikabila, mapigano yaliyosababisha vifo vya watu wengi.