Watanzania waishio China watakiwa kufanya kazi kwa bidii

0
2303

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka
Watanzania wanaoishi nchini China kufanya kazi kwa bidii na kuchangamkia fursa zilizopo nchini humo.

Akizungumza na Watanzania hao jijini Beijing, Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka kuhakikisha wanazitangaza vema fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania.

Amesema kuwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi na kufanya shughuli mbalimbali wana nafasi kubwa na muhimu katika kuiletea nchi yao maendeleo.

Waziri Mkuu Majaliwa yuko nchini China kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuanza Septemba Tatu mwaka huu jijini Beijing na kufunguliwa na Rais Xi Jinping wa China.

Waziri Mkuu Majaliwa anamuwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo.