Shambulio la kujitoa muhanga lasababisha shule kuporomoka

0
2287

Kumetokea shambulio la kujitoa muhanga katika ofisi moja ya serikali kwenye mji mkuu wa Somalia, – Mogadishu na kusababisha shule iliyokuwa karibu na ofisi hiyo kuporomoka.

Mtu aliyekua kwenye gari amejilipua katika eneo la ofisi hiyo na kusababisha askari watatu kuuawa na watu wengine 14 kujeruhiwa wakiwemo watoto Sita.

Askari hao waliouawa walikua wakijaribu kulizuia gari hilo lililokuwa limejaa milipuko kuingia kwenye ofisi hiyo ya serikali.

Shambulio hilo pia limeharibu nyumba zilizo karibu na ofisi hiyo na kung’oa paa la msikiti mmoja.

Wanamgambo wa Al-Shabab ambaao wamekuwa wakifanya mashambulio mbalimbali kwa zaidi ya miaka 10 nchini Somalia wamedai kuhusika na tukio hilo.