Wananchi wa mkoa wa Irnga tangu kuanza kutekelezwa kwa agizo la serikali la kuzuia matumizi ya mifuko hiyo June mwaka huu.
Taarifa hiyo imetolewa wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira duniani iliyofanyika kimkoa katika viwanja vya mashujaa mkoani Iringa.
Nusu tani ya Mifuko ya plastiki maarufu kama Rambo kutoka kwa wafanyabiashara na wananchi wa kawaida wa Iringa, imekusanywa na kukabidhiwa kwa Mkuu wa mkoa huo Ally Hapi kwa lengo la kuiteketeza kwa utaratibu maalum bila kuleta madhara.
Siku hii ya mazingira imeambatana na maoneshoya bidhaa za mifuko mbadala ya karatasi ambapo vikundi kadhaa vya wanawake vimejitokeza kutumia fursa ya kutengeneza mifukohiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi amezishauri Halmashauri za wilaya mkoani kuviwezesha vikundi vya wanawake, vijanana walemavu vilivyoonyesha nia ya kuwekeza katika utengenezaji wa mifuko ya karatasi kwakuwa nunulia mashine za kazihiyo.
