Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini- CGF, Thomas Andengenye amesema katika kughamua matukio ya moto, wameanzish kampeni za kuwa na klabu katika shule za bweni.
Amesema hayo katika ziara yake mkoani Ruvuma,akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Kamishna Jenerali wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini- CGF, Thomas Andengenye amesema hatua ya awali ni kufundisha moto usitokee.
Katika hatua nyingine Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji amesema kufahamu changamoto za jeshi hilo inasaidia kukabiliana nazo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thomas Andengenye ameyasema hayo alikuwa katika ziara ya ukagzui wa kazi zinazofanywa na kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoani Ruvuma
