Marekani yafuta msaada wa kijeshi kwa Pakistan

0
2284

Marekani imetangaza kufuta msaada wa Dola Milioni 300 za Kimarekani kwa Pakistan kwa madai kuwa nchi hiyo imeshindwa kuyachukulia hatua makundi ya wanamgambo.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Marekani imesema kuwa nchi hiyo itatumia fedha hizo kwa masuala mengine ya dharura.

Marekani imesema kuwa Pakistan imekuwa ikipuuza ama kushindwa kukabiliana na wanamgambo wanaoendesha shughuli zao kwenye ardhi ya nchi hiyo wakiwemo wanamgambo wa Haqqani na wale wa Talibabn.

Mwezi Januari mwaka huu Marekani ilisema kuwa itafuta karibu misaada yote ya shughuli za ulinzi kwa nchi hiyo ya Pakistan.