Viwavi jeshi vamizi na mbegu zisizo stahimili magonjwa na hali ya hewa ni baadhi ya changamoto kubwa zinazoendelea kuumiza vichwa vya wataaalumu nchini ilikutafuta njia bora ya kukabiliana na tatizo hilo .
Utafiti wa awali uliofanywa na wataalamu na watafiti wa chuo kikuuu cha sokoine cha kilimo sua morogoro umebaini mmea wa muarobaini na mlonge unaweza kudhibiti viwavi jeshi vamizi katika mazao ikiwemo mahindi.
Mhadhiri wa chuo kikuu kutoka SUA ,Dr Newton Kilasi amesema kukamilika kwa utafiti huo kutawezesha wakulima wengi zaidi kutumia mimea hiyo na kuachana kutumia viuatilifu vyenye madhara kwa mazao na ardhi.
Vilevile Dr Newton Kilasi anaeleza namna walivyoamua kushirikiana na shirika la kilimo endelevu SAT kufanya tafiti zitakazo wasaidia wakulima wadogo wadogo kukabiliana na tatizo hilo huku mtafiti Martha Agustino akieleza utafiti huo unavyoendelea kufanyika
Baadhi ya wakulima walitembelea vitalu vya utafiti kwa lengo la kujionea matumizi ya mimea hiyo wakaeleza namna wanavyokabilina na viwavi jeshi vamizi sambamba na mwezeshaji kutoka shirika la SAT Elizabeth Girangai akilezea matarajio yao.