Maelfu ya watu Argentina waandamana

0
522

Maelfu ya watu katika mji wa Buienos Aires nchini Argentina,  wameshiriki katika maandamano ya kupinga serikali ya nchi hiyo  kutokana na hatua yake ya kubana matumizi kupita kiasi, hali ambayo wanasema inafanya maisha yao kuwa magumu.

Huduma mbalimbali nchini Argentina zikiwemo shule na shughuli za kibiashara zimelazimika kufungwa, huku idadi kubwa ya watu wakishiriki katika maandamano hayo, na wananchi wakisema kuwa wamechoshwa na serikali ya nchi hiyo.

Argentina imekuwa ikishuhudia mdororo wa uchumi, licha ya kuwa na rasilimali mbalimbali, hali inayowatia hasira Raia wa nchi hiyo.

Baadhi ya watu katika mitaa mbalimbali ya mji wa Buinos Aires, wamepika chakula na kukigawa bure kwa waandamanaji, ikiwa ni hatua ya kushikamana wanaposhiriki katika maandamano hayo.