Serikali ya Israel imejikuta njia panda baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo kutoka chama cha Likud, -Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda serikali kwa sababu mbalimbali.
Netanyahu amekuwa akimshutumu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Israel wakati wa serikali yake iliyopita kuwa chanzo cha tatizo hilo, kwani haonyeshi utayari wa kuunganisha vyama vingine vya siasa ili hatimaye kuundwa kwa serikali mpya.
Chama cha Netanyahu licha ya kushinda katika uchaguzi mkuu uliomalizika nchini humo, lakini hakikuweza kupata viti vya kutosha kukiwezesha kuunda serikali.
Chama hicho kinalazimika kuungana na vyama vingine ili hatimaye kiweze kuunda serikali.
Hata hivyo Netanyahu amekuwa akishutumiwa na baadhi ya watu nchini humo kuwa alikuwa akijihusisha na vitendo vya rushwa.
Wanasiasa nchini humo wamekuwa wakishinikiza mwanasiasa huyo kuondolewa kinga ili aweze kushitakiwa.