Arsenal wamepoteza nafasi ya kurejea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, baada ya kufungwa mabao manne kwa moja na Chelsea katika mchezo wa fainali ya michuano ya Ligi ya Yuropa.
Mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Olympic mjini Baku nchini Azerbaijan, ulitawaliwa kwa kiasi kikubwa na Chelsea ambao wamejipatia mabao yake kupitia kwa Olivier Giroud, Pedro na Eden Hazard aliyefunga mabao mawili
Huo unakuwa ubingwa wa tano kwa Chelsea katika michuano ya vilabu Barani Ulaya, wakiwa timu ya pili kutoka England kushinda mataji mengi kwenye michuano hiyo nyuma ya Liverpool walioshinda mataji nane.
Arsenal wao wanapoteza fainali ya nne kati ya tano walizocheza kwenye mashindano ya vilabu Barani Ulaya, wakipoteza fainali ya kombe la washindi mwaka 1995, kombe la UEFA mwaka 2000, Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mwaka 2006 na michuano ya Yuropa mwaka huu wa 2019.
