Michuano ya tenisi ya wazi ya Ufaransa, – Roland Garros inaendelea kushika kasi, ambapo Gael Monfils amemtandika Mjapani Taro Daniel kwa seti tatu kwa bila ya 6-0, 6-4, 6-1.
Naye Adrian Mannarino amemchapa Stefano Travaglia kwa seti tatu kwa moja kwa ushindi wa 6-7, 6-3, 3-6, 6-2, 6-2 huku Zverev akimchapa John Millman kwa seti tatu kwa moja ya 7-6 6-3, 2-6, 6-7 6-3.
Muangentina Del Potro amemfunga Nicolas Jarry kwa seti tatu kwa moja kwa ushindi wa 3-6, 6-2, 6-1, 6-4 na Fabio Fognini amefunga Andreas Seppi kwa seti tatu kwa moja ya 6-3, 6-0, 3-6, 6-3.
