Watoto Ishirini kufanyiwa upasuaji wa Moyo

0
429

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es salaam, – Profesa  Mohamed Janabi amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wa bodi ya shirika la Okoa Moyo wa Mtoto – Save a Child’s Heart (SACH) la nchini Israel.

 Mazungumzo hayo yamefanyika huku kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku Saba ikiendelea katika Taasisi hiyo ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Wakati wa kambi hiyo, watoto 20 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo kwa kuziba matundu yaliyopo kwenye moyo,  na kuzibua mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo.