Mabweni ya Sekondari ya Ashira yateketea kwa moto

0
491

Mabweni mawili katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Ashira iliyopo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro yameteketea kwa moto.

Mabweni hayo yanayojulikana kama bweni la Japan na bweni la Muungano yanayokaliwa na  Wanafunzi 297,  yameteketea kwa moto wakati wanafunzi wakiwa darasani huku wanafunzi 73 vitu vyao vyote vikiteketea.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Moshi ambaye pia ni Mkuu wa wilaya hiyo Kippi Warioba amesema kuwa bado chanzo cha moto huo hakijajulikana, lakini wamefanikiwa kuuzima moto huo  kwa wakati kwa kushirikiana wanafunzi na kikosi cha zimamoto.

Kippi amesema kuwa zoezi la tathmini linaendelea ili kujua thamani ya vitu vilivyoteketea kwa moto na pia kujua chanzo cha moto huo.