IGP Sirro akagua ujenzi JNIA

0
247

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, – Simon Sirro ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Tatu la abiria katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kilichopo jijini Dar es salaam.

Akiwa katika eneo hilo la ujenzi, IGP Sirro amepatiwa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo na Msimamizi wa mradi huo Mhandisi Barton Komba ambaye amesema kuwa hadi sasa ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 99.

Akizungumza mara baada ya kupatiwa taarifa hiyo, IGP Sirro amesema kuwa Jeshi la Polisi Nchini limejipanga ili kuimarisha usalama katika kiwanja hicho.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi Nchini,  pia amefanya ziara ya kukagua Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)  Ukonga jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amezungumza na Maofisa na Askari wa kikosi hicho.