Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pallangyo, ameapishwa hii leo Bungeni jijini Dodoma kushika rasmi wadhifa huo.
Dkt Pallangyo alitangazwa rasmi kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye jimbo hilo la Arumeru Mashariki mwezi Aprili mwaka huu.