Mbunge Masele aitikia wito wa Spika

0
377

Kamati ya Kinga, Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge  imekutana jijini Dodoma kwa lengo la kumhoji Makamu wa kwanza wa Rais  wa Bunge la  Afrika, – Stephen  Masele ambaye amerejea nchini kutoka nchini Afrika kusini baada Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kumtaka afanye hivyo ili ahojiwe na kamati hiyo kwa kile kinachodaiwa kutumia nafasi yake vibaya kuchafua taswira ya nchi .

Masele ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) alifika katika viwanja vya Bunge majira ya asubuhi na kuingia katika ukumbi wa Bunge ambapo mkutano wa 15 wa Bunge hilo unaendelea.