Rais Magufuli atoa zawadi katika mashindano ya kusoma Quran

0
285

Rais Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI  ameongoza maelfu ya wananchi na viongozi mbali mbali wa serikali na dini  katika mashindano maalum ya 20 ya kuhifadhi  Quran Tukufu Afrika  yaliyofanyika  katika uwanja wa Taifa jijini DSM.

Jumla ya washiriki 20 kutoka mataifa 18 wameshiriki mashindano hayo ambapo  Mshindi wa mashindano hayo amezawadiwa shilingi Milioni 20 za kitanzania..

Viongozi wengine wastaafu waliohudhuria tukio hilo ni marais wastaafu wa Tanzania, Dkt. JAKAYA KIKWETE na ALHAJ ALI HASSAN MWINYI ambaye ni mlezi wa mashindano hayo.

Nae Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi Bin ALI ameipongeza Taasisi hiyo kwa kufanikisha mashindano hayo  ambayo lengo lake ni kuwalea watoto katika maadili mema kumjenga mtu kuwa na maadili mazuri

Pia Rais Magufuli ameiagiza TAMISEMI kutoa kibali cha kutoa eneo waliloomba taasisi ya Al Hikma katika manispaa ya Temeke  kupewa eneo hilo kwa ajili ya kujenga hospitali.

Nae msimamizi wa taasisi ya Al hikma Sheikh Nurdin Kishk amewataka viongozi barani afrika kuiga mfano wa Rais wa Tanzania katika umoja, upendo na ushirikiano anaouonyesha kwa dini mbalimbali nchini.