Vicent Kompany kuaga Manchester City baada ya kudumu kwa miaka 11

0
277

Nahodha wa MANCHESTER CITY Vicent Kompany {33} ameaga rasmi kuitumikia klabu hiyo baada ya kuiongoza timu hiyo kutwaa taji la Kombe La Chama Cha Soka ENGLAND- FA baada ya kupata ushindi wa mabao SITA kwa BILA dhidi ya WATFORD katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa kwenye dimba la WEMBLEY.

Mabao ya DAVID SILVA, RAHEEM STERLING aliyefunga mabao MATATU , KEVIN DE BRUYNE na GABRIEL JESUS yametosha kuwapa ushindi huo MANCHESTER CITY ambapo sasa wanaweka rekodi yao mpya kwa kutwaa mataji yote ya ndani pale ENGLAND, ikiwa ni timu ya kwanza kufanya hivyo.

Wababe hawa tayari ni mabingwa wa kombe la Ligi maarufu kama CARABAO walilolitwaa mwezi FEBRUARI kwa ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penalty dhidi ya CHELSEA, Ligi Kuu ya ENGLAND na sasa Kombe la FA. Kompany amecheza jumla ya michezo 360 na kufunga mabao 20.