Armensty International yashutumu uhalifu Libya

0
436

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu  la Armensty International limesema kuwa lina ushahidi wa kutosha kuwa vitendo vya uhalifu wa kivita vimetekelezwa nchini Libya, baada ya nchi hiyo kujikuta katika mapigano mapya.

Libya imejikuta katika mapigano mapya, baada ya mbabe wa kivita nchini humo Khalifa Haftar kutangaza kuwa anaelekea mjini Tripoli  kutokomeza vikundi vya kigaidi nchini humo, huku askari wake wakitangaza kuwa wanakwenda kutwaa madaraka.

Kwa wiki Sita sasa, majeshi ya serikali ya mpito ya Libya yamekuwa yakipambana na wapiganaji wa Haftar, ambao baada ya kuona kuwa wanazidiwa nguvu, wamekuwa wakifanya mashambulio dhidi ya raia mjini Tripoli.